Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka wauaji Nepal wafikishwe mbele ya sheria

UM wataka wauaji Nepal wafikishwe mbele ya sheria

Shirika la Umoja wa Mataifa linalopigania uhuru wa vyomvo vya habari leo limesema linataka wauaji wa mmiliki wa vyomvo vya habari nchini Nepal na wanaotoa vitosho dhidi ya waandishi wa habari wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.

Kauli hiyo imetolewa kwa nia ya kulinda maslahi ya vyombo vya habari ambavyo ni muhimu kwa upashaji huru wa habari na kuchagiza mijadala.

Jamim Shah, Mkuu wa kituo cha satellite cha televishen ya Nepal na kampuni ya Cable televishen ya Space Time Network, alipigwa risasi na kuuawa na watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki mjini Katmandu tarehe 7 ya mwezi huu. Dereva wake aitwaye Mathuraman Malakar alijeruhiwa vibaya katika tukio hilo.