Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madaktari wanahofu idadi ya vifo kuongeza Haiti

Madaktari wanahofu idadi ya vifo kuongeza Haiti

Wafanyakazi wa huduma za dharura wanaonya kwamba idadi ya vifo huwenda ikaongezeka kutokana na watu walojeruhiwa vibaya sana na kutopata matibabu yanayohitajika.

Watalamu wanasema vituo vya afya vingali na orodha ya watu ambao bado hawakupata tiba kwa siku 12, wakati wagonjwa wanazidi kuwasili na makambi ya kiholela yenye maelfu ya walonusurika huweza yakazusha magonjwa. Dk Greg Elder naibu mkurugenzi wa kazi za shirika la madaktari wasio na mipaka huko Haiti anasema, kitisho kikubwa cha afya ni kuzuka ugonjwa wa kuharisha, magonjwa ya kuambukiza ya mapafu na magonjwa mengine miongoni mwa maelfu ya watu wanaoishi katika makambi yaliyojazana watu, bila ya huduma za usafi.