Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Ijumanne, wawakilishi wa kutoka Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) walitiliana sahihi na Serikali ya Sudan makubaliano ya jumla kuhusu mradi wa utendaji, uliokusudiwa kuhakikisha usalama wa watumishi wa UNAMID pamoja na mali zao. Taadhima ya utiaji sahihi mapatano haya ilifanyika kufuatilia kikao cha utendaji kazi, kilichokutana Khartoum Ijumapili ya tarehe

 20 Disemba 2009, ambapo wawakilishi wa makundi mawili husika - UNAMID na Serikali - walijadilia uwezo na njia za kuchukuliwa pamoja, kupunguza mashambulio dhidi ya wafanyakazi wa UNAMID. Kwa mujibu wa taarifa za UM, mnamo miezi ya karibuni vitendo vya kuteka nyara wafanyakazi na magari ya UNAMID, ikijumlisha na ongezeko la mashambulio ya kuvizia, vilikithiri katika Darfur. Liuteni-Jenerali Patrick Nyamvumba, Kamanda Mkuu wa Vikosi vya UNAMID alitia sahihi makubaliano ya kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wa UNAMID na Liuteni-Jenerali Magzoub Rahma, Mkurugenzi wa Kitengo cha Ushirkiano wa Kiamataifa kwenye Wizara ya Ulinzi. Kamanda Mkuu wa UNAMID alisema itifaki yao hii itaimarisha mapatano yaliopo hivi sasa juu ya Hadhi-ya-Sheria-ya-Vikosi vya UNAMID (SOFA), kanuni ambayo itawapatia "hatua ziada za kusitisha ule mwelekeo, unaozidi kupanuka, wa hali isiyo salama katika Darfur." Mapatano yaliosahihiwa yataidhinishwa rasmi baada ya wiki mbili. Kwa mujibu wa mfumo wa SOFA, jukumu kubwa muhimu linalohusu usalama na hifadhi ya walinzi amani wa UNAMID, pamoja na hifadhi ya mali zao, lipo chini ya serikali mwenyeji ya Sudan.