Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Baraza la Usalama Alkhamisi liliendeleza shughuli zake, awali, kwa kuzingatia taarifa mpya ya Kamati ya Vikwazo kuhusu azimio 1737, linaloambatana na "uzuiaji wa uenezaji wa silaha za kinyuklia na Iran." Balozi Yukio Takasu wa Ujapani, mwenyekiti wa kamati, aliwakilisha ripoti kwenye Baraza. Baada ya hapo, Mwakilishi Mtendaji wa KM kwa Burundi, Youssef Mahmoud alihutubia Baraza la Usalama na kuelezea kupatikana kwa maendeleo ya kutia moyo kwenye mpango wa amani na katika matayarisho ya uchaguzi wa 2010 nchini Burundi. Alisema kuna matatizo kidogo kuhusu msaada wa fedha zinazohitajika kusimamia uchaguzi ujao, kwa sababu alisema mataifa kadha yalioahidi kuchangisha fedha za kuendesha uchaguzi hayajatimiza ahadi zao bado. Baadaye, Baraza la Usalama liliendeleza majadiliano juu ya Burundi kwenye kikao cha faragha.

Ahmedou Ould-Abdallah, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, ametoa mwito maalumu unaosihi wahusika wote kusitisha machafuko na vurugu nchini Usomali, hali ambayo alisema iliangamiza na kuharibu maisha ya fungu kubwa la raia katika Usomali. Ould-Abdallah alitangaza mwito huo kwa kuambatana na taadhima ya Siku ya Haki za Binadamu. Alikumbusha juu ya msiba uliotukia wiki iliopita mjini Mogadishu wakati wa sherehe za kutoa shahada kwa wanafunzi waliohitimu masomo ya udaktari, kutokana na shambulio la bomu la kujitoa mhanga. Shambulio liliangamiza maisha ya mawaziri wa serikali, madaktari na wanafunzi wa utabibu, marafiki na aila zao pamoja na kuua walimu na waandishi habari. Ould-Abdallah alisema msiba wa tukio hilo liliozuka tarehe 03 Disemba unaodhihirisha namna Wasomali wanavyowatenda ndugu zao. Aliwasihi Wasomali waliopo nchini na wale waliotawanyika mataifa ya nje, kulaani vikali na kupinga vitendo vyote vya vurugu na machafuko, na kuhimiza waongeze maradufu bidii za kurudisha utulivu na amani nchini mwao.

Karine AbuZayd, Kamishna Mkuu wa Shirika la UM Linalofarajia Wahamiaji wa Falastina katika Mashariki ya Karibu (UNRWA), leo alizuru nyumba ya mmoja wa aila za KiFalastina wliofukuza kutoka makazi halai yao kutoka eneo la Sheikh Jarrah katika Jerusalem Mashariki. Familia nane sasa hivi zinakabiliwa na hatari ya kulazimishwa kuondoka kwenye nyumba zao, kwa amri ya taifa liliokalia kimabavvu maeneo yao la Israel. AbuZatd alisema UM unakana kabisa madai ya Israel ya kuwa uamuzi wa kuwan'goa WaFalstina kutoka majumbani mwao ni masuala yanayohusu manispaa na mahakama za kienyeji, vitendo ambavyo alikumbusha vinaharamisha majukumu ya Israel chini ya sheria ya kimataifa. Alkumbusha wiki iliopita KM alitoa risala iliosema "alipigwa na mshangao" juu ya kuendelea kwa vitendo vya kubomoa makazi ya WaFalastina, kuwatoa kwa mabavu majumbani mwao na badala yake kwaweka walozweei za Kiisraili. AbuZayd alisema walionyanganywa kwa nguvu mali zao nq kung'olewa makazi ni lazima kutambuliwa na wapatiwe haki kutokana na dhulma na uonevu dhidi yao. Alisema amani inaweza kuwasilishwa kwenye eneo hilo la Masahriki ya Kati pindi Mataifa Wanachama yatasisitiza na kuhishimu ubinadamu wetu sote.