Skip to main content

Baraza la Usalama limelaani ongezeko la mashambulio ya LRA katika JKK

Baraza la Usalama limelaani ongezeko la mashambulio ya LRA katika JKK

Ijumanne asubuhi, Baraza la Usalama lilifanyisha mashauriano kuhusu masuala ya eneo la Maziwa Makuu na tatizo la waasi wa Uganda wa kundi la LRA.

... Naibu KM juu ya Masuala ya Kisiasa, B. Lynn Pascoe aliwakilisha taarifa maalumu mbele ya wajumbe wa Baraza, iliochanganua maendeleo kuihusu mada mbili hizo. Baraza la Usalama lilitarajiwa kupitisha taarifa ya Raisi kwa vyombo vya habari juu ya masuala hayo mawili. Vile vile Baraza lilitazamiwa, wakati ninalekea studio, kusailia mada nyengine zinazoambatana na usalama na amani, ambapo Tiébilé Dramé, mjumbe maalumu wa UM, alitazamiwa kutoa taarifa kuhusu maendeleo katika mvutano wa kisiasa nchini Bukini.