Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama Maalum juu ya Makosa ya Vita katika Sierra Leone imekataa rufaa ya wahukumiwa waasi wa RUF

Mahakama Maalum juu ya Makosa ya Vita katika Sierra Leone imekataa rufaa ya wahukumiwa waasi wa RUF

Hukumu ya mwisho ya Mahakama Malumu juu ya Makosa ya Vita katika Sierra Leone, imeidhinisha adhabu iliopitishwa kabla, dhidi ya viongozi watatu wa kundi la waasi la RUF, iendelee kutekelezwa kwa kulingana na makosa waliotuhumiwa nayo, ikijumlisha makosa ya kufanyisha ndoa za kulazimishwa, kitendo ambacho kilitafsiriwa kuharamisha ubinadamu, na vile vile yale makosa ya kuhujumu walinziamani wa kimataifa - na hii ni mara ya kwanza kwa mahakama za kimataifa kuchukua hatua hii ya kisheria. Mahakama ya Maalumu ya Sierra leone ilikataa kabisa maombi yote ya rufaa ya washtakiwa, isipokuwa ombi moja la mtuhumiwa Agustine Gbao, ambaye hapo kabla alishtakiwa kuendeleza adhabu za jamii, hukumu ambayo ilibatilishwa. Hata hivyo, Gbao ataendelea kutumikia kifungo cha miaka 25 gerezani.

Watuhumiwa wawili wengine waliopewa adhabu ya kifungo cha muda mrefu na Mahakama ni Issa Sesay, ambaye alishtakiwa kifungo cha miaka 52 pamoja na Morris Kallon, anayetazamiwa kutumikia kifungo cha miaka 40. Kesi iliobakia ya makosa ya vita katika Sierra Leone ni ile ya aliyekuwa Raisi wa Liberia Charles Taylor, ambayo bado inaendelea mjini Hague, Uholanzi kwa hivi sasa.