Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM inaadhimisha Siku Kuu ya Kuwahishimu Watu Waliozeeka

UM inaadhimisha Siku Kuu ya Kuwahishimu Watu Waliozeeka

Tarehe ya leo, Oktoba 01, inaadhimishwa na UM kuwa ni Siku ya Kimataifa kwa Watu Waliozeeka. Kwenye risala aliotuma KM kuihishimu siku hii, alitoa mwito maalumu uitakayo walimwengu kukomesha tabia ya kubagua wazee wenye umri mkubwa.

Vile vile alipendekeza vitendo vya udhalilishaji wa watu wazee usitishwe, halan, pamoja na kukomesha utumiaji mabavu dhidi yao na tabia ovu ya kutowajali fungu hili la jamii ya kimataifa.