Mashambulio ya kikabila Sudan Kusini yalaaniwa na KM

Mashambulio ya kikabila Sudan Kusini yalaaniwa na KM

KM ameshtumu vikali shambulio liliotukia mwisho wa wiki liopita katika Sudan kusini, ambapo iliripotiwa watu 100 ziada waliripotiwa kuuawa, ikiwa miongoni mwa msururu wa mapigano ya kikabila yaliopamba karibuni kwenye eneo hili la Sudan.

Kadhalika, iliripotiwa nyumba 2,000 zilichomwa moto na watu wenye bunduki baada ya kumaliza kushambulia kijiji cha Duk Padiet, kwenye jimbo la Jonglei mnamo asubuhi ya tarehe 20 Septemba (2009). KM aliisihi Serikali ya Sudan Kusini kuongeza jitihadi za kuwatambua na kuwafikisha mahakamani wakosaji wa uhalifu huo. Kwa hivi sasa, KM ameinasihi Serikali ya Sudan Kusini kujaribu kurudisha tena utulivu kwenye eneo la uhasama, na kuhakikisha mashambulio ya kulipiza kisasi hayatoruhusiwa kutukia kieneo, na pia kuyahimiza makundi husika kushiriki kwenye mazungumzo ya upatanishi ili kusuluhisha mvutano wao.