Shughuli za "kufufua amani" Sierra Leone zaashiriwa kukabiliwa na vizingiti ziada kwa siku zijazo
Baraza la Usalama asubuhi lilikutana kuzingatia juu ya shughuli za Ofisi ya Muungano wa Huduma za Ujenzi Amani katika Sierra Leone (UNIPSIL).
Michael von der Schulenberg, Mjumbe Mtendaji wa KM kwa Sierra Leone, aliwatahadharisha wajumbe wa Baraza kwamba licha ya kuwa Sierra Leone imeshaanza safari ya kutia moyo ya kurudisha utulivu, amani na mfumo wa demokrasia nchini, safari hii inaendelea kukabiliwa na vizuizi kadha wa kadha, na inabashiriwa itakuwa refu, na wakati mwengine hata kuwa safari ya hatari. Alisema wanachohitajia wazalendo wa Sierra Leone kwa sasa hivi ni wakati zaidi pamoja na subira na uongozi ulio imara na shupavu vitu ambavyo, kwa msaada ziada kutoka jumuiya ya kimataifa, watafanikiwa kuimarisha amani ndani ya nchi.