Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa za wiki kuhusu maambukizo ya H1N1 duniani

Taarifa za wiki kuhusu maambukizo ya H1N1 duniani

Kwenye taarifa iliotangazwa Geneva asubuhi ya leo, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilibainisha takwimu mpya juu ya vifo vinavyotokana na maambukizi ya janga la virusi vya homa ya mafua ya A/H1N1 katika dunia, ambapo iliripotiwa jumla ya vifo vilivyosajiliwa rasmi kutokana na maradhi hayo kwa sasa katika vizio vya dunia vyote viwili, vya kaskazini na kusini, halkadhalika, ni sawa na watu 2,873.