Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID imepokea maofisa polisi ziada kutoka Nepal na Nigeria

UNAMID imepokea maofisa polisi ziada kutoka Nepal na Nigeria

Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) limepokea maofisa wa polisi 26 kutoka Nepal na polisi 30 wa Nigeria waliowasili kwenye mji wa El Fasher leo Ijumatatu.

Kuwasili kwa polisi hawa katika Darfur kutajumlisha maofisa 3,000 ziada watakaoenezwa katika sehemu kadha za jimbo la magharibi la Sudan kuimarisha utulivu na usalama. Kadhalika, Ijumamosi iliopita, watumishi raia wa kimataifa wawili wanaofanya kazi na UNAMID - mwanamme mmoja na mwanamke mmoja - walitoroshwa kwa kushikiwa bunduki, kutoka nyumbani mwao katika Zalingei, Darfur Magharibi, na watu wanne/watano waliokuwa wamechukua silaha. Watumishi hawa wa UNAMID wamechukuliwa kwenye sehemu zisiojulikana. Wenye madaraka Sudan wamesharifiwa juu ya tukio hili na wamehaidi kuwa watachukua hatua zote zinazohitajika kuhakikisha watumishi wa UNAMID wanarejeshwa kwenye mastakimu yao salama.