Wazalendo wa JKK wahitajika kukuza maendeleo na kupiga vita rushwa, asihi Doss

Wazalendo wa JKK wahitajika kukuza maendeleo na kupiga vita rushwa, asihi Doss

Alan Doss, Mjumbe Maalumu wa KM kwa JKK, Ijumatatu aliwaambia wajumbe waliowakilisha jumuiya za kiraia, waliohudhuria mkutano uliofanyika mjini Kinshasa kusailia masuala ya usalama na amani nchini, kwamba wakati umewadia kwa wananchi kutekeleza mageuzi ya kizalendo kwenye zile juhudi za kupiga vita umaskini na ulaji rushwa katika taifa lao.

Aliwakumbusha kwamba UM upo tayari, kusaidia kwenye kadhia hizi muhimu pindi wadau wote husika watabuni miradi yenye uwezo hakika wa kukuza uchumi na kupunguza hali duni katika JKK.