Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa Huduma za Dharura ahimiza ushirikiano ziada kukidhi mahitaji ya dharura Sudan

Mkuu wa Huduma za Dharura ahimiza ushirikiano ziada kukidhi mahitaji ya dharura Sudan

John Holmes, Naibu KM juu ya Misaada ya Dharura na Masuala ya Kiutu amemaliza ziara ya siku tano Sudan mwisho wa wiki.

Lengo hasa la ziara lilikuwa ni kufanya mapitio juu ya mahitaji ya kiutu, hasa kwenye yale maeneo yalioathirika na uamuzi wa Serikali ya Sudan uliotangazwa tarehe 04 Machi, wa kuyafukuza nchini mashirika yasio ya kiserikali 13 na kusitisha shughuli za mashirika yasio ya kiserikali ya kizalendo. Holmes alisema ana matarajio ushirikiano mpya baina ya serikali na jumuiya inayohudumia misaada ya kiutu katika Sudan itawasilisha imani mpya miongoni mwa makundi yote husika. Mkuu huyu wa UM anayehusika na misaada ya dharura, ya kiutu, alipongeza ahadi aliyopokea kutoka Serikali ya Sudan kwamba itaimarisha  ushirikiano na jumuiya ziziso za kiserikali, katika kuhudumia mahitaji ya kiutu, kwa muda mfupi na katika muda mrefu, kwenye yale maeneo ya mzozo. Misaada ya UM inafungamana na huduma za kuupatia umma muhitaji chakula, lishe bora, uangalizi wa afya, makazi ya muida, maji safi na vile vile usafi wa mazingira na mastakimu kwa waathirika wa mizozo.