Takwimu ziada juu ya tetemeko la ardhi Utaliana

Takwimu ziada juu ya tetemeko la ardhi Utaliana

Ripoti za Ofisi ya UM juu ya Misadaa ya Dharura (OCHA) pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO) zinakadiria idadi ya vifo vnavyoambatana na zilzala kali iliopiga karibuni kwenye eneo la kati, na katika mji wa L\'Aquila, Utaliana limefikia 207.

Watu 1,500 waliripotiwa kujeruhiwa na tetemko hilo la ardhi, na makazi ya watu 17,000 yameharibiwa. Kadhalika, vikundi vya waokoaji wanaohusika na huduma za dharura walifanikiwa kuwatoa hai kutoka vifushi watu 150 ambao walinusurika maisha.