Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM yafungua vituo viwili vya uwokozi Bahari ya Hindi

UM yafungua vituo viwili vya uwokozi Bahari ya Hindi

Shirika la kimataifa la Safari za Baharini la UM IMO limefungua vituo viwili vipya vidogo vya kutafuta na kuokoa maisha ya watu baharini huko Tanzania na Ushelsheli, njee ya pwani ya Afrika ya Mashariki.

Katika mkutano wa mwisho wa IMO 2000, serekali za nchi za Kiafrika ziliidhinisha azimio linaloalika mataifa yote yanayopakana na bahari ya Atlantic na Bahari ya Hindi, kuanzia Morocco hadi Somalia na visiwa vya karibu kufungua vituo vitano vya kutafuta na uwokozi baharini na vituo 26 vidogo kuhudumia maeneo yote ya pwani ya Afrika. Vituo hivyo viwili vidogo vitafanya kazi kwa ushirikiano na kituo cha Kuratibu Uwokozi Baharini huko Mombasa kilichofunguliwa kwanza mwezi May 2006.