Mjumbe Maalum wa UM apongeza juhudi za Uganda na Kongo dhidi ya waasi

16 Machi 2009

Wanajeshi wa Uganda walianza kurudi nyumbani siku ya Jumapili kutoka JKK, baada ya operesheni ya pamoja ya miezi mitatu na jeshi la nchi na lile la kusini mwa Sudan, kuwafurusha wapiganaji wa kundi la Lord Resistance Army LRA.

Mjumbe maalum wa UM huko JKK, Alan Doss amesifu operesheni hiyo iliyopewa jina la Lightening na Thunder, lakini wakati huo huo kuonya kwamba kundi hilo lingali kitisho katika eneo hilo. Mjumbe huyo anaiongoza afisi ya UM MONUC, anasema operesheni hiyo kwa wakati huu imekamilika, lakini alisisitiza kwamba kungali kuna makundi kadhaa ya LRA yaliyobaki, hiyo ikimanisha kuna kazi zaidi yakufanya kuwalinda raia. Bw Doss alikua akizungumza kwenye sherehe za kukamilisha operesheni hiyo ya kijeshi zilizohudhuriwa na wanadiplomasia, mawaziri na wakuu wa kijeshi kutoka nchi zote mbili.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter