Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuungana na mabingwa wa kandanda Ulaya kupambana na nja

UM kuungana na mabingwa wa kandanda Ulaya kupambana na nja

Mabingwa wakuu wa kandanda huko Ulaya pamoja na mamilioni ya mashabiki wao wana lengo la kupachika goli dhidi ya njaa kote duniani katika kampeni ya kwanza kabisa kote Ulaya, ili kuhamasisha mzozo wa njaa unaowakumba watu bilioni moja.

Hayo yameelezwa na shirika la Chakula na Kilimo la UM FAO. Zaidi ya vilabu 200 kutoka ligi kuu za Ulaya zitacheza michuano yake hapo Machi 20 hadi 22 kama sehemu ya kampeni ya "Wachezaji waKulipwa wa Kandanda dhidi ya Njaa".