Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM Ban na Rais Obama wajadili kuimarisha uhusiano kati ya UM na Marekani

KM Ban na Rais Obama wajadili kuimarisha uhusiano kati ya UM na Marekani

KM Ban Ki-moon na Rais Barrack Obama wa Marekani wamekubaliana juu ya umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Marekani na UM walipokutana Ijumanne huko Washington.

Wakizungumza na waandishi habari baada ya mkutano wao katika ikulu ya White House, Bw Ban alisema UM na Marekani zina mawazo na malengo sawa juu ya amani, utulivu, maendeleo na haki za binadamu.

Anasema anadhani mwaka 2009 ni mwaka wa mafanikio au kushindwa, kukiwa na mizozo katika kila upande inayokabili UM, Marekani na jumuia ya kimataifa kwa ujumla.

Bw Ban aliwasili Washington akitokea Port-au-Prince ambako amehimiza kufanyike mageuzi ya kisiasa na kiuchumi katika taifa hilo la Haiti, moja wapo maskini kabisa duniani. Alisema nchi hiyo ni moja wapo ya change moto kubwa zinaowakabili viongozi wa dunia. Kwa upande wake rais Obama alisema alizungumza masuala mbali mbali ya kimataifa na KM, ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa, Afghanista, na Sudan. Alisema Hali huko Sudan imezidi kua mbaya.

"Serekali ya Khartoum imeyafukuza baadhi ya makundi muhimu kabisa ya kutoa huduma za dharura kwa mamilioni ya watu nchini humo. Huu ni mzozo mkubwa zaidi kuliko Tulivyotarajia."

Huu ulikua mkutano wa kwanza kati ya viongozi hao wawili, na kila mmoja alisisitiza nia ya kufanya kazi pamoja. KM aliendelea na ziara yake ya Washington Jumatano kwa kukutana na Kamati ya Maswala ya Mambo ya Nje ya Mabaraza Mawili ya Bunge la Marekani. Na baadae mchana alikutana na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Hillary Clinton.