Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wamulika athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa afya

Wataalamu wamulika athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa afya

Athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa afya, ni suala muhimu ambalo wapanga sera wanabidi kuzingatia na kufahamu wanapopanga vipau mbele vya maendeleo na uwekezaji.

Wameeleza hayo waatalamu wa Shirika la Afya Duniani katika mkutano juu ya Hatari za Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani huko Copenhagen. Kufuatana na takwimu za WHO, vifo vya watu elfu 150 hutokea sasa kila mwaka katika mataifa yenye mapato ya chini, kutokana na mambo manne muhimu yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Upungufu wa mazao na utapia mlo, magonjwa ya kuharisha, malaria na mafuriko. Waatalamu wanasema kuimarisha hali ya mazingira na kupunguza utowaji wa gesi za carbon kunaweza kupunguza janga la magonjwa duniani kwa asili mia 25.