Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yaonya dawa sugu kutishia juhudi za kupambana na Malaria

WHO yaonya dawa sugu kutishia juhudi za kupambana na Malaria

Shirika la Afya duniani WHO limesema jumatano kwamba kujitokeza kwa dawa iliyo sugu dhidi ya ugonjwa wa Malaria huko Kusini Mashariki ya Asia inaweza kuhujumu vibaya sana mafanikio ya kimataifa katika kuudhibiti ugonja huo.

Kufuatana na habari zilizotolea na shirika hilo huko Geneva, kuna ushahidi mpya ya vijidudu ambavyo vinakaidi artemisinin dawa muhimu inayotumiwa kutibu ugonjwa huo kwenye maeneo ya mpaka kati ya Cambodia na Thailand ambako wafanyakazi hutembea kwa miguu kwa mili kadhaa kila siku kwenda kufyeka misitu. Naibu mkurugenzi wa WHO, Dr Hiroki Nakatani amesema, ikiwa hawatizuia hali hii ya dawa sugu dhidi ya malaria huko kwnye mpaka wa Cambodia na Thailand, inaweza kusamba kwa haraka hadi nchi jirani na kutishia juhudi za kuudhibiti ugonjwa huo wa hatari unaoua. WHO inaeleza kwamba mchanganyiko wa madawa ya Artemisinin au ACT, umeweza konekana kua ni mafanikio makubwa kabisa katika kutibu malaria, ikifanikiwa karibu kwa asili mia 90.