Skip to main content

Mjumbe maalum wa UM awataka wanamgambo wa Kihutu kuondoka Kongo

Mjumbe maalum wa UM awataka wanamgambo wa Kihutu kuondoka Kongo

Mjumbe maalum wa UM huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amewahimiza tena wapiganaji wa kihutu kutoka Rwanda katika jimbo lenye misukosuko la Kivu ya Kaskazini, kuweka chini silaha zao na kurudi nyumbani.

Bw Alan Doss, mjumbe maalum wa KM huko DRC amesisitiza kwamba ni lazima kwa wanamgambo wa kundi la FDLR wajiunge kwa hiyari mpango wa kuwapokonya silaha, kuwarudisha nyumbani na kujiunga tena na jamii DDRRR, unaongozwa na afisi ya UM huko DRC, MONUC. Bw Doss, alisema inabidi wapiganaji hao wafahamu kwamba hawakaribishwi tena katika ardhi ya Kongo, na kwamba maelfu ya raia wakimbizi wameamua kurudi nyumbani kupitia msaada wa shirika la UM la kuwahudumia wakimbizi, UNHCR. Mjumbe huyo alikua anazungumza baada ya ziara ya siku mbili huko Kivu ya kaskzini kutathmini mashmabulizi ya pamoja ya kijeshi kati ya serekali ya DRC na jeshi la Rwanda yenye lengo la kuliondowa kundi la FDLR kutoka eneo hilo. Bw Doss alifuatana na mwakilishi mpya wa UNHCR katika kanda hiyo, Mohamed Boukkry na Jenerali Bipin Rawat kamanda wa kikosi cha MONUC huko Kivu ya Kaskazini, na kiutembelea mji wa Pinga, ambako kikosi cha UM kina kambi na kushirikiana na jeshi la Congo kuwalinda raia.