Skip to main content

Majeshi ya AU na UM yaimarisha doria kuwalinda waliopoteza makazi yao

Majeshi ya AU na UM yaimarisha doria kuwalinda waliopoteza makazi yao

Kikosi cha pamoja cha Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa huko Darfur UNAMID kimeripoti leo kwamba kikosi chake cha polisi kitafanya doria ya kwanza wakati wa usiku kutokea kituo kipya cha polisi katika jamii CPC kilichojengwa kati kati ya makambi mawili makubwa ya watu walopoteza makazi yao IDP\'s karibu na mji wa El Fasher mji mkuu wa Darfur ya Kaskazini.

Ujumbe wa wakazi kambi ya El Salaam wamewashukuru polisi wa UNAMID kwa msaada wao katika kuachiliwa huru baadhi ya wakazi wa kambi hiyo walokua wamewekwa kizuizini na maafisa wa ujasusi wa serekali ya Sudan. Kufuatana na UNAMID, ujenzi wa kituo kingine cha polisi CPC karibu na kambi ya Zamzam, utanza mnamio wiki mbili zijazo, katika kambi tofauti ya wa IDPs huko El Fasher. Hatua hiyo inayoanza usiku wa leo inamaanisha kwamba polisi wa UNAMID watapiga doria katika eneo hilo katika operesheni ya masaa 24 mfululizo kama sehemu ya kuimarisha ulinzi kwa wakazi karibu elfu kumi wanaopatiwa hifadhi katika kambi za Abu Shouk na El salaam.