Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM yarudia mwito wa kuachiwa afisa aliyetekwa nyara Pakistan

UM yarudia mwito wa kuachiwa afisa aliyetekwa nyara Pakistan

UM umerudia tena mwito wake wa kutaka kuachiliwa kwa afisa mmoja wa UM aliyetekwa nyara huko kusini magharibi ya Pakistan.

 John Solecki Mmarekani, ambae ni mkuu wa Shirika la kuwahudumia wakimbizi la UM UNHCR katika mji wa Quetta, mji mkuu wa jimbo la Balochistan, alitekwa nyara na washambulizi wasojulikana mapema mwezi huu. Taarifa ya UM inaeleza kwamba, ina wasi wasi mkubwa juu ya hali ya afya ya Solecki ambayo inasemekana inazidi kua mbaya. UM kwa mara nyingine tena imetoa mwito kwa mateka wa John kuwasiliana moja kwa moja au kupitia mpatanishi wa kuaminika ili kuweza kutanzua tatizo hilo kwa njia ya amani.