Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA juu ya Operesheni za Amani kwa Darfur (UNAMID) vimeripoti kuwa mashambulizi bado yanendelea Ijumatano ya leo katika eneo la Muhajeriya. Ripoti pia imedai vikosi vya Serikali ya Sidan vilionekana vikifanya doria kwenye eneo liliopo karibu mita 500 kutokea kambi ya UNAMID. Kadhalika iliripotiwa, ndege isiotambulikana, ilionekana kutupa mabomu matatu hii leo, kilomita moja kutoka majengo ya UNAMID pamoja na mashambulizi yaliosababisha raia kukimbilia kwenye kambi za vikosi mseto vya kimataifa. Kambi ya wahamiaji wa ndani ya Al Salaam, katika Darfur Kaskazini imepokea wahamaji wapya 520 wakati Kambi ya Wahamiaji ya Zam Zam ilipokea wahajiri 1,400 waliokuwa wakitafuta hifadhi kutoka vurugu liliofumka karibuni kwenyeeneo lao. UNAMID inasema asilimia 90 ya wahamiaji wapya wa ndani hujumlisha wanawake na watoto wadogo, jamii ambayo imepatiwa mahema ya kujistiri.

Kikao cha 47 cha Kamisheni ya UM kuhusu Maendeleo ya Jamii kilifunguliwa rasmi Ijumatano asubuhi kwenye Makao Makuu ya UM. Mkutano ulifunguliwa bia na Balozi Sylvie Lucas wa Luxembourg, aliye Raisi wa Baraza la UM juu ya Uchumi na Jamii pamoja na Sha Zukang, Naibu KM juu ya Masuala ya Uchumi na Jamii. Mada inayofanyiwa mapitio na kikao cha mwaka huu cha Kamisheni inahusu ‘Fungamano za Kijamii’ kwa miaka ya 2009-2010, na vile vile duru ya sera zinazoambatana na uhusiano uliopo baina ya juhudi za kukomesha ufukara na umaskini. Kadhalika mapitio yatafanyiwa zile sera zinaohusu maandalizi ya ajira kamili kwa wote na kazi inayohishimika. Mijadala ya Kamisheni itasailia namna mzozo wa uchumi wa dunia unavyoathiri huduma za maendeleo na kutafuta taratibu za kujikomboa na tatizo hili. Mwenyekiti wa Kamisheni ya Maenddeleo ya Jamii ni Balozi Kirsti Lintonen wa Finland.