Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukulima shadidi lazima urekibishwe kutimiza mahitaji ya chakula kwa vizazi vijavyo, asema mtaalamu wa FAO

Ukulima shadidi lazima urekibishwe kutimiza mahitaji ya chakula kwa vizazi vijavyo, asema mtaalamu wa FAO

Mtaalamu wa mimea kutoka Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) aliwaambia wajumbe karibu 1,000 waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Nne wa Kutunza Kilimo Bora, unaofanyika wiki hii kwenye mji wa New Delhi, Bara Hindi, kwamba mahitaji ya chakula kwa umma wa kimataifa unaoendelea kuongezeka, kwenye mazingira yalioathirika na mabadiliko ya hali ya hewa, mahitaji hayatoweza kutimizwa bila ya kwanza kurekibisha mifumo ya ukulima shadidi, inayotumiwa hivi sasa kimataifa.