Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO ina matumaini viwavi haribifu Liberia vitadhibitiwa

FAO ina matumaini viwavi haribifu Liberia vitadhibitiwa

Timu ya wataalamu wa sayansi wa Shirika la FAO waliozuru, wiki iliopita, maeneo saba ya Liberia, kufanya utafiti kuhusu aina ya viwavi haribifu vilivyopamba nchini humo, leo wametangaza matokeo ya uchunguzi wao yaliosisitiza kwamba mripuko wa vijidudu haribifu hivyo, unaweza kudhibitiwa, kwa urahisi zaidi, kinyume na zile taarifa za siku za nyuma.