Hapa na Pale

20 Januari 2009

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Eneo la MAziwa Makuu, Olusegun Obasanjo, Ijumanne alikutana na Raisi Joseph Kabila mjini Kinshasa katika JKK. Raisi Kabila alimweleza Mjumbe wa KM juu ya operesheni zinazoendelezwa shirika, sasa hivi, ndani ya nchi na majeshi ya JKK na Rwanda, dhidi ya kundi la waasi la FDLR. Operesheni hii zinatarajiwa kuendelea kwa wiki kadhaa zijazo. Vile vile mazungumzo ya kisiasa ya kudumisha suluhu ya amani kwenye Eneo la Maziwa Makuu, hususan katika sehemu ya mashariki katika JKK, bado yanaendelea chini ya usimamizi shirika wa Mjumbe Maalumu wa KM, Obasanjo na Raisi Mstaafu wa Tanzania Bejamin Mkapa. ~

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Eneo la MAziwa Makuu, Olusegun Obasanjo, Ijumanne alikutana na Raisi Joseph Kabila mjini Kinshasa katika JKK. Raisi Kabila alimweleza Mjumbe wa KM juu ya operesheni zinazoendelezwa shirika, sasa hivi, ndani ya nchi na majeshi ya JKK na Rwanda, dhidi ya kundi la waasi la FDLR. Operesheni hii zinatarajiwa kuendelea kwa wiki kadhaa zijazo. Vile vile mazungumzo ya kisiasa ya kudumisha suluhu ya amani kwenye Eneo la Maziwa Makuu, hususan katika sehemu ya mashariki katika JKK, bado yanaendelea chini ya usimamizi shirika wa Mjumbe Maalumu wa KM, Obasanjo na Raisi Mstaafu wa Tanzania Bejamin Mkapa.

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kwamba raia waliong’olewa makazi, kutokana na mashambulio ya mara kwa mara ya waasi wa Uganda wa LRA waliojibanza kwenye sehemu za JKK, wanakabiliwa kwa sasa na matatizo magumu ya chakula, ukosefu wa makazi ya muda, madawa, nguo na vifaa vyengine vya dharura. Kwa asababu ya kuwepo barabara mbaya kwenye maeneo ya uhasama, UM unashindwa kugawa misaada ya kihali kwa umma muathirika katika JKK. Katika siku za karibuni waasi wa LRA wameanza tena kuhujumu na kuwashambulia raia wa JKK katika eneo la Haut Uele. UNHCR inakadiria katika miezi mine iliopita watu 135,000 waling’olewa makazi katika JKK kwa sababu ya mashambulio ya waasi wa LRA, hali ambayo vile vile ilisababisha watu 560 kuuawa na waasi.

Ahmedou Ould-Abdallah, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, amehimiza Serikali ya Mpito pamoja na wawakilishi wa Umoja wa Ukombozi Mardufu wa Usomali kuendelea na utekelezaji kamili wa Mapatano ya Djibouti. Alisema Kamati ya Kiwango cha Juu ya makundi husika na mzozo wa Usomali inakutana sasa hivi Djibouti kujadilia suala la kupanua uwakilishi wakatika Bunge na kuunda serikali ya muungano. Vile vile wajumbe wa kimataifa wamewakilishwa kwenye mazungumzo ya Djibouti.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter