Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa KM anaamini upanuzi wa viti bungeni Usomali unaashiria utulivu

Mjumbe wa KM anaamini upanuzi wa viti bungeni Usomali unaashiria utulivu

Ahmedou Ould-Abdallah, Mjumbe Maalumu wa UM kwa Usomali, amenakiliwa akisema kwamba ana “matumaini makubwa” kuhusu maendeleo ya kurudisha utulivu na amani katika Usomali, kufuatia uamuzi wa asilimia kubwa ya wawakilishi wa bunge wa Serikali ya Mpito, wa kuongeza viti vipya 275 bungeni.