Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMIS yakanusha uvumi wa kuhamisha wafanyakazi kufuatia uamuzi wa ICC

UNMIS yakanusha uvumi wa kuhamisha wafanyakazi kufuatia uamuzi wa ICC

Kadhalika kuhusu Sudan, Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani Sudan Kusini (UNMIS) Ijumapili limetangaza taarifa yenye kukana uvumi unaonenzwa na magazeti ya Sudan, kwamba UM unadhamiria kuhamisha watumishi wa kimataifa na wale wa kizalendo, kutoka Sudan kwa kukhofia karibuni Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC) huenda ikapitisha hati ya kuwashika baadhi ya viongozi wa Sudan, ikijumlisha Raisi Omar al-Bashir, kwa madai walishiriki kwenye makosa ya vita, pamoja na kushiriki kwenye mauaji ya halaiki katika Darfur.