Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR inasailia majaaliwa ya wahamiaji wa Kisomali katika Kenya

UNHCR inasailia majaaliwa ya wahamiaji wa Kisomali katika Kenya

Mapema wiki hii Shirika la UNHCR liliripoti wasiwasi wake kuhusu taarifa ilizopokea zilizothibitisha kwamba Serikali ya Kenya huwarejesha makwao kwa nguvu makwao,wale wahamiaji wa Kisomali wenye kuomba hifadhi ya kisiasa.

“Tukio la karibuni lilijiri wiki iliopita, pale wenye madaraka

Kenya walipoamua kuwarejesha makwao, kwa nguvu, Wasomali watatu walioomba hifadhi ya kisiasa, walioingia nchini Kenya kwa kupitia sehemu ya mpakani ya Liboi, iliopo kaskazini-mashariki ya nchi.” Alisema wahamiaji hawa watatu, wakijumuisha mwanamke mmoja na wanaume wawili, walikuwa miongoni mwa kundi la Wasomali kadha ambao gari lao lilizingiwa na polisi wa mpakani, pale lilipoingia nchini mnamo tarehe 16 Januari (2009). Kwa mujibu wa taarifa za UNHCR, maofisa wa mipakani Kenya walidai dereva wa gari husika alikataa kusimama pale alipoamrishwa kusimama, kitendo kilichowafanya polisi kufyatua risasi na kuwajeruhi abiria watatu. Majeruhi hawa watatu walichukuliwa kutoka eneo la mpakani la Liboi na walipelekwa kwenye kambi ya wahamiaji ya Dadaab, iliopo kilomita 90 ambapo walipatiwa matibabu. Ama kuhusu abiria wengine 26 waliokuwa kwenye gari na majeruhi majaaliwa yao hayajulikani sasa hivi na UNHCR.

UNHCR imeripoti kwamba wahamiaji majeruhi watatu walipohojiwa wakati wakipatiwa matibabu kwenye mji wa Dadaab walisema walikimbia mapigano yaliofumka karibuni kwenye mji wa Mogadishu na wakaamua kuomba hifadhi ya kisaiasa Kenya. UNHCR iliomba rasmi wahamiaji hawa majeruhi wakabidhiwe Idara ya Masuala ya Wahamiaji ya Kenya. Kwa mujibu wa ripoti za hospitali, mnamo tarehe 21 Januari polisi sita wa Kenya walikwenda kwenye Kituo cha Afya cha Dadaab, walipotibiwa majeraha ya risasi wale wahamiaji wa Kisomali watatu, na kuwachukua na kuwatia ndani ya karandinga, na baadaye kuwarudisha Usomali, kitendo ambacho kilithibitishwa na polisi.

UNHCR imeiarifu serikali ya Kenya kuhusu tukio hili, pamoja na matukio mengine kama hayo yanayohusu Wasomali walioomba hifadhi ya kisiasa katika mwaka 2008, ambao pia walirejeshwa kwa nguvu Usomali. UNHCR iliwakumbusha wenye madaraka Kenya jukumu lao, chini ya Mkataba Geneva wa 1951 pamoja na Sheria ya Kenye kuhusu Wahamiaji ambayo hairuhusu kitendo cha kuwarejseha makwao kwa nguvu wale wageni wenye kuomba hifadhi ya kisiasa. UNHCR ilisihi Kenya kuendelea kutekeleza sheria za kuwalinda wahamiaji ambazo zimeshaidhinishwa rasmi na Serikali.