Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua ziada zahitajika kudhibiti kipindupindu Zimbabwe, inasema WHO

Hatua ziada zahitajika kudhibiti kipindupindu Zimbabwe, inasema WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa mwito muhimu wa kutaka kuchukuliwa hatua ziada, za haraka, kudhibiti kipindupindu nchini Zimbabwe, maradhi ambayo bado yanaendelea kutesa raia kwa kasi kuu.

“Hali ni ya kutia wasiwasi, maana jumla ya wagonjwa wa kipindupindu sasa hivi imeshakiuka 60,000, na hiki ni kiwango kikubwa kabisa cha maambukizo, hali ambayo haionyeshi dalili ya kupungua, na tunakhofia itaendelea kupamba ndani ya nchi.” Alisema vile vile WHO inaashiria janga la maradhi litafurika na kusambaa hata kwenye mataifa jirani. Alikumbusha pia kwamba idadi ya vifo vya kipindupindu bado inapanda .. na tangu mwezi Agosti 2008 wagonjwa 3,100 wameshafariki kwa maradhi hayo. Alisisitiza Dktr Laroche ya kwamba bila ya kuchukuliwa hatua za dharura kimataifa kudhibiti kipindupindu katika Zimbabwe, maradhi yataselelea na kuendelea kuathiri taifa hilo na vile vile mataifa jirani.