Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM ahimiza mchango ziada wa mataifa tajiri kuimarisha maendeleo ya nchi maskini

KM ahimiza mchango ziada wa mataifa tajiri kuimarisha maendeleo ya nchi maskini

Kwenye mkutano na waandishi habari uliofanyika Davos, Uswiss, KM Ban Ki-moon alitoa mwito maalumu wenye kusihi mataifa matajiri kutowasahau wanadamu wenziwao katika nchi maskini, hasa katika kipindi ambacho maendeleo ya uchumi yamepwelewa na yanaendelea kuporomoka duniani.

KM aliwaambia waandishi habari waliokusanyika kwenye Mkutano wa Uchumi wa Dunia uliofanyika Davos, Uswiss ya kuwa kunahitajika kuwepo ushirikiano mpya kwenye juhudi za kusukuma mbele miradi ya maendeleo, ili kukuza vyema uchumi wa mataifa maskini, pamoja na kukidhi mahitaji ya afya ya maeneo hayo,na kuondosha umaskini uliokithiri na njaa.