Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa mpya ya WHO juu ya kipindupindu Zimbabwe

Taarifa mpya ya WHO juu ya kipindupindu Zimbabwe

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti hali ya afya ya jamii katika Zimbabwe inaanza kudhibitiwa hivi sasa, kufuatilia miripuko ya wiki za karibuni, ya magonjwa ya kipindupindu.

“Maeneo matatu yalioathirika vibaya zaidi na miripuko ya kipindupindu yalikuwa mji mkuu wa Harare ambapo watu 6488 (elfu sita mia nne themanini na nane) waliambukizwa maradhi hayo na 179 (mia moja sabini na tisa) walifariki; jimbo la pili lilioathirika sana na kipindupindu lilikuwa lile eneo la Bay Bridge, ambapo watu 3190 (elfu tatu mia moja na tisini) waliambukizwa na ugonjwa huo na kusababisha vifo vya watu 83 (themanini na tatu), ikifuatiwa na mji wa Mudzi ambapo watu 1234 (elfu moja mia mbili na thelathini na nne) nawo walipatwa na kipindupindu, na kati ya jumla hiyo watu 57 (khamsini na saba) walifariki. Vile viel tumepokea taarifa ya kuzuka kipindupindu katika sehemu ya mji ulio karibu na mpaka na Botswana, na katika wilaya ya Guro, ndani ya taifa la Msumbiji. Hali hii ya kufumka kwa maradhi inatokana na sababu kadhaa, ikijumuisha ukosefu wa maji safi na salama, na vile vile uhaba wa usafi wa mazingira, hasa ilivyokuwa katika siku za karibuni kutokana na migomo ya wafanyakazi katika sekta ya afya, ambao hawajalipwa mishara kitambo, wafanyakazi waliopo kudhibiti huduma za afya na usafi, kwa kuondoa maji machafu na takataka, ni wachache sana.”