Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchina yapeleka manowari mbili mwambao wa Usomali kupambana na maharamia

Uchina yapeleka manowari mbili mwambao wa Usomali kupambana na maharamia

Imeripotiwa leo hii kwamba manowari mbili za Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Uchina, pamoja na meli moja iliobeba shehena za kukidhi mahitaji ya wanamaji, zimeanza safari ya kuelekea kwenye eneo la mwambao wa Usomali kujiunga na manowari za mataifa mengine wanachama wa UM, kwa madhumuni ya kukabiliana na maharamia waliopamba karibuni katika sehemu hiyo ya Pembe ya Afrika.

“Kama mwanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama, Uchina imedhaminiwa majukumu makubwa ya kuimarisha usalama na amani ya kimataifa.” Alisema hatua hii ya hadhari iliochukuliwa na taifa lake kupeleka manowari Usomali inatokana na mapendekezo ya maazimio kadha ya Baraza la Usalama, na kwa mujibu wa hatua husika zinazotekelezwa na nchi nyengine wanachama katika UM … kadhia ambayo inachangisha juhudi za pamoja za jumuiya ya kimataifa, zenye dhamira hakika ya kupambana na vitendo vya uharamia katika mwambao wa Usomali, na inamaanisha Uchina nayo imejiunga, kihakika, kutekeleza majukumu yenye kusaidia kuimarisha utulivu kwenye uhusiano wa kimataifa. Alisema Balozi Zhang Yesui taifa lake limenuia kuyatekeleza maazimio ya UM pamoja na sheria za kimataifa dhidi ya vitendo vya uharamia katika Usomali, na anaamini manowari za Uchina zitatekeleza operesheni zake kwa mafanikio na bila ya matatizo.