Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tetesi za Al-Jazeera juu ya UNMIS na ICC hazina msingi, inasema UM

Tetesi za Al-Jazeera juu ya UNMIS na ICC hazina msingi, inasema UM

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani Sudan Kusini (UNMIS) imetoa taarifa yenye kukanya tetesi zilizochapishwa kwenye magazeti ya Khartoum, yakinakili shirika la habari la Al-Jazeera ambalo lilidai Mjumbe Maalumu wa KM kwa Sudan, na Mkuu wa UNMIS, Ashraf Qazi, alibashiria tarehe ya uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa juu ya Makosa ya Jinai ya Halaiki (ICC) kuhusu maombi ya kushikwa Ahmed Harun, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Sudan na ambaye sasa ni Waziri wa Nchi juu ya Masuala ya Kiutu, pamoja na Ali Kushayb, kiongozi wa jeshi la mgambo la Janjaweed.