Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR ina wasiwasi juu ya kupotea kwa wahamiaji wa ndani 50,000 katika JKK

UNHCR ina wasiwasi juu ya kupotea kwa wahamiaji wa ndani 50,000 katika JKK

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kupotea idadi ya wahamiaji wa ndani 50,000 ambao hawajulikani walipo, kufuatia kuchomwa moto vituo vya makazi ya muda viliopo mji wa Rutshuru, katika Kongo mashariki.

"wingi wao wataogopa kurejea vijijini kwao, kwa sababu walihama kutoka makazi hayo karibu mwaka mzima sasa; na wengine wapo mbali na kambi za wahamiaji, na hawana fununu yoyote nini cha kutarajia pindi wataamua kurejea kwenye maeneo hayo.” UNHCR inaamini fungu kubwa la wahamiaji waliopotea hivi sasa wanakaa, ama na marafiki, au jamaa; na baadhi yao wanaishi kwenye makanisa kutafuta hifadhi, na katika majumba mengine ya kiraia. Redmond pia alisema baadhi yao wanafikiriwa walielekea Uganda, na wengineo ziada huenda wakawa pia wanaelekea mipakani huko. Alisisitiza itachukua muda kujua kihakika wahamiaji wa ndani waliopokea wamelekea wapi hasa hivi sasa. Kadhalika, UNHCR inajaribu kuhudmia misaada ya kihali wahamiaji 135,000 waliopo kwenye zile kambi sita zinazosimamiwa na UM katika maeneo ya karibu na Goma.