Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walimwengu wahishimu Siku ya Kisukari Duniani

Walimwengu wahishimu Siku ya Kisukari Duniani

Tarehe ya leo, Novemba 14, inahishimiwa na UM kuwa ni Siku ya Kukumbushana Maradhi ya Kisukari Duniani. Walimwengu huiadhimisha siku hii kwa kushirikiana kwenye kampeni kadha wa kadha za kuamsha hisia za umma wa kimataifa juu ya namna ya kujikinga na ugonjwa huu wa kisukari.