Skip to main content

Wakulima maskini watafadhiliwa misaada ya kumudu madhara ya hali ya hewa

Wakulima maskini watafadhiliwa misaada ya kumudu madhara ya hali ya hewa

Mashirika mawili ya UM – yaani Shirika juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) na Shirika la Mfuko wa Kimataifa juu ya Maendeleo ya Kilimo (IFAD) – yametangaza kuchangisha juhudi zao kipamoja na Wakf wa Bill na Melinda Gates kuwapatia msaada wa fedha wa dola miloni moja, wakulima maskini wanaokabiliwa na athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa pamoja maafa ya kimaumbile katika mataifa yanayoendelea.