Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UM Usomali asihi viongozi wa kitaifa waungane

Mjumbe wa UM Usomali asihi viongozi wa kitaifa waungane

Ahmedou Ould-Abdallah, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali leo ametoa taarifa inayowanasihi viongozi wa Usomali, kutoka sekta zote za kitaifa, [pamoja na] wale waliopo nchi za kigeni, kuweka kando mifarakano na tofauti za kiitikadi baina yao, na kuwahimiza waungane, kipamoja, kusaidia kuimarisha utulivu na amani ya taifa lao, hasa katika kipindi ambapo Siku Kuu ya Eid al Adh’ha inakaribia.