UM yasaidia kupiga vita maradhi yanayoua migomba Afrika Mashariki
Mradi wa pamoja uliotekelezwa na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) na serikali ya Uganda, umewasaidia wakulima 3 000 kupambana na ugonjwa uliohatarisha kuangamiza uzalishaji wa mavuno ya ndizi za kupikia, zao kuu kwa raia milioni 14 wa Uganda ambao hulitegemea kwa mapato na chakula.