Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bidhaa za Afrika hazina thamani kwenye soko la kimataifa, imeonya UNCTAD

Bidhaa za Afrika hazina thamani kwenye soko la kimataifa, imeonya UNCTAD

Ijumatatu, Shirika la UM juu ya Maendeleo na Biashara (UNCTAD) limewasilisha rasmi ripoti mpya kuhusu athari za uregezaji wa shuruti na kanuni za biashara kuhusu bidhaa za Afrika katika soko la kimataifa. Ripoti ilipewa mada isemayo Maendeleo ya Uchumi Afrika kwa 2008.

Ripoti ya UNCTAD imependekeza Afrika ifadhiliwe mchanganyiko wa viambato vya kutosha vitakavyoyasadia mataifa kupata fursa ya kuuza bidhaa zao, kwa wingi zaidi, na bila vizingiti kwenye soko la dunia. Ripoti ilionya maendeleo yamepwelewa katika uuzaji wa bidhaa za Afrika nje, na yapo nyuma sana tukilinganisha na mataifa mengine yanayoendelea. Ripoti ilisisitiza Afrika kuweza kufanikiwa kuuza kwa wingi bidhaa zao nje italazimika kuwapatia wafanyakazi mafunzo ya kisasa, na kuhakikisha huduma za umeme zinaaminika, kuwa na fursa za kufanya utafiti wa maendeleo, na kunakuwepo uekezaji unaokubali mageuzi na mabadiliko, hasa kwenye huduma za benki, na pia kuhakikisha kunakuwepo usafiri ulio imara ambao bei zake huwa ni za ushindani, na kuzalisha idadi kubwa ya bidhaa zinazohitajika kuridhisha matakwa ya wanunuzi kwenye soko la kimataifa.