Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mukhtasari wa Mkutano wa Norway kwa Wanaharakati Vijana Kutunza Mazingira

Mukhtasari wa Mkutano wa Norway kwa Wanaharakati Vijana Kutunza Mazingira

Mkutano wa Watoto wa Kimataifa wa Tunza unaofanyika kwenye mji wa Stavanger, Norway kuanzia tarehe 17 hadi 21 Juni uliandaliwa na Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) pamoja na Shirika lisio la Kiserekali la Norway linaloitwa Ajenda ya [Karne ya] 21 kwa Vijana, wakichanganyika na wafadhili wengine wa kimataifa. Mkutano ulikusanyisha vijana 700 wa umri kati ya miaka 10 mpaka 14, wakiwakilisha zaidi ya nchi 100, ambao waliongozwa na watu wazima 300.

Nilipata fursa ya kuwahoji, kwa simu, wawakilishi vijana watatu kutoka Kenya na Tanzania ambao walitupatia maoni yao kuhusu mkutano na kuzngumzia mchango wao kwenye huduma za kudhibiti bora mazingira nchini kwao.

Sikiliza mahojiano yetu kwenye idhaa ya mtandao.