Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

BU lakutana katika kikao muhimu kuzingatia Kosovo

BU lakutana katika kikao muhimu kuzingatia Kosovo

Baraza la Usalama limekutana Ijumaa, kwenye kikao maalumu, kusailia ripoti ya karibuni ya KM kuhusu hadhi ya operesheni za ulinzi wa amani za UM katika Kosovo.

Kikao cha Baraza la Usalama kilihudhuriwa na Raisi wa Serbia, Boris Tadic na vile vile ujumbe wa Kosovo ulioongozwa na Raisi Fatmir Sejdiu.