Mtaalamu wa UM anahimiza juhudi ziongezwe kusaidia IDPs Kenya
Hivi karibuni, Walter Kaelin, Mjumbe wa KM juu ya Wahamiaji wa Ndani Waliong’olewa Makwao, au Wahamiaji wa IDPs, alizuru Kenya kwa siku nne kutathminia hali ya wale watu waliohamishwa makazi kwa nguvu kutokana na vurugu liliozuka nchini kufuatilia uchaguzi wa taifa mnamo mwisho wa 2007.