Skip to main content

Juhudi za UM kuishawishi Myanmar kupokea misaada ya kiutu ya kimataifa

Juhudi za UM kuishawishi Myanmar kupokea misaada ya kiutu ya kimataifa

Ijumapili mataifa zaidi ya 50, yalihudhuria kikao maalumu mjini Yangon, Myanmar, kilichotayarsihwa kidharura na Wanachama wa Umoja wa Mataifa ya Kusini ya Asia (ASEAN) kwa makusudio ya kuchangisha fedha za kusaidia kihali fungu kubwa la umma wa Myanmar uliodhuriwa na Kimbunga Nargis kilichopiga huko tarehe pili Mei.

KM Ban Ki-moon katika risala alioitoa mbele ya wajumbe wa kimataifa waliohudhuria mkutano wa Yangon alisema kunahitajika mchango wa dola milioni 200 kwa sasa ili kuwasaidia waathiriwa wa Kimbunga Nargis kupata huduma za kimsingi katika miezi sita ijayo. Kwa mujibu wa ripoti aliotuma mwandishi habari wa Redio ya UM, Maoqi Li, alipokuwa Yangon, aliarifu KM Ban pia aliahidi yeye binafsi kufuatilia maafikiano yake na Kiongozi wa Myanmar kwa kuhakikisha juhudi za kimataifa zitatekelezwa haraka na hazitopwelewa.

Sikiliza ripoti kamili kwenye idhaa ya mtandao.