Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Kufyeka Tumbaku Duniani yaadhimishwa kimataifa

Siku ya Kufyeka Tumbaku Duniani yaadhimishwa kimataifa

Tarehe 31 Mei huadhimishwa kila mwaka na UM kuwa ni Siku ya Kukomesha Matumizi Hatari na Maututi ya Tumbaku Duniani.

Kwa hivyo WHO imetoa mwito maalumu, na muhimu, wenye kupendekeza kwa serikali za kimataifa kupiga marufuku haraka aina zote za matangazo ya bishara yanayoambatana na bidhaa za tumbaku na ufadhili wa kadhia hiyo, kwa kuhakikishapia kuwa kunakuwepo mazingira huru yalioepukana na madhara ya tumbaku.