Skip to main content

Siku ya UM Kuwakumbuka Waathiriwa wa Utumwa Duniani - Balozi wa Tanzania anasailia maana hakika ya siku hii kwa Afrika

Siku ya UM Kuwakumbuka Waathiriwa wa Utumwa Duniani - Balozi wa Tanzania anasailia maana hakika ya siku hii kwa Afrika

Mnamo tarehe 25 Machi mwaka huu, kwa mara ya kwanza katika historia ya UM, kulifanyika hafla maalumu kwenye Makao Makuu mjini New York, kuheshimu Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka Waathiriwa wa Janga la Utumwa na Biashara ya Utumwa katika Bahari ya Atlantiki.

Taadhima hizi ziliandaliwa shirika na Wanachama wa Jumuiya ya Mataifa ya Karibian (CARICOM), wawakilishi wa Umoja wa Afrika pamoja na Ubalozi wa Marekani katika UM, na vile vile Idara ya Habari kwa Umma ya UM (DPI).

Tanzania hivi sasa imekabidhiwa madaraka ya Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, taasisi ambayo iliwasilishwa kwenye hafla za UM za kuwakumbuka waathiriwa wa utumwa wa Atlantiki na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika UM, Balozi Augustine Mahiga. Redio ya UM ilifanya mahojiano maalumu na Balozi Mahiga ambapo alitupatia fafanuzi za mtazamo wa mataifa ya Afrika kuhusu siku ya kumbukumbu za ‘makovu ya utumwa’ ilioandaliwa na UM, na athari zake kwa vizazi husika.

Sikiliza ripoti kamili kwenye idhaa ya mtandao.