Skip to main content

Ziara ya kutathminia amani Burundi imeakhirishwa na UM baada ya kuzuka mapigano

Ziara ya kutathminia amani Burundi imeakhirishwa na UM baada ya kuzuka mapigano

Ofisi ya UM juu ya Ujenzi wa Amani katika mataifa yaliopitia hali ya vurugu na mapigano, imearifu Serikali ya Burundi kwamba imeamua kuakhirisha ziara ya tume maalumu iliyokusudiwa kuelekea Burundi mwisho wa wiki iliopita, kutathminia taratibu za kufufua na kuimarisha shughuli za kurudisha utulivu na amani nchini humo.