Skip to main content

UM kuiadhimisha rasmi Siku ya Malaria Duniani

UM kuiadhimisha rasmi Siku ya Malaria Duniani

Kikao cha 60 cha Baraza Kuu la Shirika la Afya Duniani (WHO), kilichofanyika Geneva mwezi Mei 2007, kilipitisha, kwa kauli moja pendekezo la kuifanya tarehe 25 Aprili kila mwaka iadhimishwe kuwa ni Siku ya Malaria Duniani. Makusudio ya pendekezo hili ni kuitumia siku hiyo kupigia mbiu ya mgambo zile juhudi za kimataifa za kudhibiti bora ugonjwa maututi wa malaria. ~

Siku ya Malaria Duniani inatarajiwa kuyapataia mataifa yalioelemewa na ugonjwa huu nafasi ya kufunzishana uzoefu uliokusanywa kwenye juhudi za kudhibiti bora malaria, na kuratibu sera za pamoja zitakzosaidia kukabiliana na magonjwa haya thakili kwa mafanikio.

Sikiliza ripoti kamili katika idhaa ya mtandao.