Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNCTAD inasema uekezaji wa vitega uchumi vya kigeni una natija nyingi kwa nchi zinazoendelea

UNCTAD inasema uekezaji wa vitega uchumi vya kigeni una natija nyingi kwa nchi zinazoendelea

Kwenye Mkutano wa XII wa Shirika la UM juu ya Maendeleo na Biashara (UNCTAD) unaofanyika Accra, Ghana kuliandaliwa warsha maalumu, uliokuwa na majadiliano mazito kwenye meza ya mzunguko, ambapo kulisailiwa ripoti ya UNCTAD iliozingatia natija za uekezaji wa moja kwa moja wa vitega uchumi vya kigeni katika nchi zinazoendelea.

Ripoti pia ilisema uekezaji huo hukuza uzalishaji katika huduma za uchumi na pia huhamasisha ujenzi mpya wa miundombinu inayohitajika kuimarisha uchumi maendeleo katika nchi masikini. Lakini natija hizi, ilionya ripoti, hazitopatikana bila ya kwanza kuandaliwa sera imara zitakazorahisisha uekezaji wa kigeni wa moja kwa moja, kadhia ambayonia lazima ichungwe ili kuhakikisha masilahi ya umma yanahifadhiwa katika kuendeleza uhusiano huu wa kiuchumi.